IBADA UBUNGO KKKT 20TH March 2016
Posted in Mahubiri on Mar 20, 2016
IBADA UBUNGO KKKT 20TH March 2016
SOMO: KANUNI YA KUMFANYA MTU AJIBIWE MAOMBI YAKE NA MUNGU
BY Mwl Giliard Summary FROM ARUSHA.
Maombi ni mazungumzo kati ya mtu na Mungu, ni njia ya mawasiliano kati ya Mtu na Mungu, na hayana mtu rasmi kwamba ni mtu fulani bali ni kwa kila mtu kwenye maisha yake
Kwa hiyo unapoingia kwenye maombi lazima uwe na kanuni(namna ya kwenda kuzungumza nae)
Asilimia kubwa ya maombi kutojibiwa iko kwa Mwanadamu na sio kwa Mungu,
Katika maisha ya kawaida kuna kanuni(protocol), za namna ya kuwasiliana
Sasa kwa Mungu kuna kanuni zifuatazo (ziko7)
1.TAFUTA KUFANANA NA MUNGU – Fanya maombi ya kutafuta mapenzi ya Mungu juu ya jambo unalotaka kuliombea, -Vua mwenendo wa kwanza,na utu wa zamani
Efeso 4:22-24 Verse 22 Mvue kwa habari ya mwenendo wa kwanza utu wa zamani, unaoharibika kwa kuzifuata tamaa zenye kudanganya; Efeso 4:22 SUV
Strip yourselves of your former nature [put off and discard your old unrenewed self] which characterized your previous manner of life and becomes corrupt through lusts and desires that spring from delusion; Ephesians 4:22 AMP
a).UOVU NA DHAMBI ZA MWANADAMU ZIMEUFICHA USO WA MUNGU
Tazama, mkono wa BWANA haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia; lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia. ISA. 59:1-2 SUV
BEHOLD, THE Lord’s hand is not shortened at all, that it cannot save, nor His ear dull with deafness, that it cannot hear. But your iniquities have made a separation between you and your God, and your sins have hidden His face from you, so that He will not hear. Isaiah 59:1-2 AMP
Kuna watu wameomba maombi kwa muda mrefu lakini bado majibu yake hayajapatikana,na pengine wameenda kwa waombaji wengi ndani na nje ya nchi,lakini bado hawajapata majibu, je ni Mungu haoni au hapendi kukusaidia?
Kwa hiyo ni vizuri KUJIULIZA MASWALI ni kwanini jambo hilo limechukua muda mrefu ili kujua tatizo ni nini, na kwa mstali huu tatizo ni UOVU na DHAMBI,
b). INGIA NDANI YA YESU ILI UFANYWE UPYA UFANANE NA YESU
Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya. 2 KOR. 5:17 SUV
c). MOYO WAKO UMPENDEZE BWANA, UMPE BWANA Na USISAHAU SHERIA YA MUNGU.
Mwanangu, nipe moyo wako; Macho yako yapendezwe na njia zangu. MIT. 23:26 SUV
Mwanangu, usiisahau sheria yangu, Bali moyo wako uzishike amri zangu. MIT. 3:1 SUV
d). – RUHUSU MUNGU AKUFANYE UPYA KATIKA ROHO YAKO NA NIA YAKO.
e) – VAA UTU UPYA ULIOUMBWA KWA NAMNA YA MUNGU KATIKA HAKI NA UTAKATIFU WA KWELI.
na mfanywe wapya katika roho ya nia zenu; mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli. EFE. 4:23-24 SUV
f) – JITAKASE NAFSI YAKO UWE MTAKATIFU KWASABABU MUNGU WAKO NI MTAKATIFU.
Kwa kuwa mimi ni BWANA, Mungu wenu; takaseni nafsi zenu basi; iweni watakatifu, kwa kuwa mimi ni Mtakatifu; wala msitie uchafu nafsi zenu kwa kitu kitambaacho cha aina yo yote, kiendacho juu ya nchi. LAW. 11:44 SUV
UTAKATIFU katika kufanana na Mungu sio swala la mjadala ni la LAZIMA, kwa hiyo ni lazima kwanza kuutafuta utakatifu kwa kujitakasa nafsi yako.
f).- UWE MTAKATIFU KWASABABU MUNGU NI MTAKATIFU
Kwa kuwa mimi ni BWANA niliyewaleta kutoka nchi ya Misri, ili kwamba niwe Mungu wenu; basi mtakuwa watakatifu, kwa kuwa mimi ni Mtakatifu. LAW. 11:45 SUV
UTAKATIFU UTAKUFANYA UMWONE MUNGU KWENYE MAOMBI YAKO. Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao; EBR. 12:14 SUV
2: JE NJIA ZAKO ZINAFANANA NA NJIA ZA MUNGU,NA JE UNA MAYUNDA YA KUMSABABISHA MUNGU AJIBU MAOMB?
Mimi, BWANA, nauchunguza moyo, navijaribu viuno, hata kumpa kila mtu kiasi cha njia zake, kiasi cha matunda ya matendo yake. YER. 17:10 SUV
a):- RUHUSU MUNGU ACHUNGUZE MOYO WAKO NA AVIJARIBU VIUNO VYAKO,
AMUA KUANZIA SASA KUWA KITEGEMEZI WA MAOMBI,AMUA KUIFUNZA KUOMBA ILI HATA USIPOPATA WATU WA KUKUSAIDIA KUOMBA BADO UWEZE KUOMBA