MAHUBIRI 04/09/2016, BY MCHG G. NKYA

Posted in Habari, Mahubiri on Sep 09, 2016


Bwana wetu Yesu Kristo apewe sifa

Wazo: Mungu hututunza kwa uweza wake NENO LUKA 7:11-17* YESU ANAMFUFUA KIJANA WA NAINA

Key Points:

  1. Katika wakati mgumu, huzuni, shida, Yesu hutokea na kusimama katikati.
  2. Yesu akisimama, shida zote hufika mwisho.
  3. Yesu aliona huzuni ya mama mjane aliyefiwa na mwanae wa pekee, akamhurumia.

Tunajifunza nini?

  1. Wewe baba au mama usimruhusu mwenzako kumnyanyasa mama mjane au yatima katika mji wako kwani utajitengenezea laana au mazingira magumu wewe na uzao wako.
  2. Tusimame na Yesu kwani tumaini lipo. Tutapita katika shida nyingi kwanza lakini tukisimama na Yesu tutaheshimiwa.
  3. Wanadamu watatuacha lakini Yesu hatatuacha.

…..Amina…..