MAHUBILI YA JUMAPILI TAREHE 30-04-2017

Posted in Habari, Mahubiri, Uncategorized on May 01, 2017


Mhubili ni Mwinjilisti Godson Mshana ,Kutoka Pugu New Land

Neno KUU:Yesu Kristo ni Mchungaji Mwena

Mistali ya kusimamia ni 1:Zaburi ya 23 2:Yohana 10:1-6 3:Ezekieli 34:11-16 4:Yeremia 33:1-

Kupitia mistali tajwa hapo juu tunajifunza mambo tofauti tofauti kwa maisha yetu kama wakristo ambao tumaini letu ni kwa bwana Yesu

i)Tunatakiwa kumtumaini Bwana Yesu na kumtegemea kama mchungaji wetu Mkuu kama alivyomwambia Yeremia

ii)Tunatakiwa kumtumaini Yesu katika changamoto tunazopitia katika maisha yetu ya kila siku,tumaini letu linatakiwa kubaki kwa Yesu tu

Yeremia japokuwa alikuwa amefungwa lakini Bwana alimwambia niite nani nitakuitikia

Sisi kama wakristo tunatakiwa kumuita Bwana katika kila jambo kila wakati naye ameahidi atatuitikia

iii)Tunaambiwa tumuite kwenye mahitaji ya KANISA,kwenye mahitaji ya KAZI,kwenye mahitaji ya FAMILIA na mambo mengine mengi

Na Mungu akubariki na apate nafasi ya kumuita kwenye maisha yako ili akuitikie kama alivyofanya kwa Yeremia

Ubarikiwe