MAHUBIRI YA TAREHE 21-01-2018 KKKT UBUNGO

Posted in Habari, Mahubiri on Jan 21, 2018


SI KILA MLANGO UNAO UONA UMEFUNGWA, NI KWELI UMEFUNGWA.

Tusome Luka 5: 1-11 Kwa kawaida ya kazi ya uvuvi hufanywa usiku. Na Simoni alijua hilo, baada ya Yesu kumwambia ashushe nyavu Simoni alisema kwa "Neno lako tutashusha" Na tunasoma muujiza waliokutana nao baada ya kutii neno la Kristo. Unapokuwa umekata tamaa na jambo lolote na Mungu akakupa maelekezo ya kufanya jambo hilohilo ambalo wewe unaona hakuna namna Jifunze "kutii neno la Kristo"

Leo hii Yesu anakuambia "Tweka mpaka kilindini ukashushe nyavu zako"

Ile biashara uliyofunga nenda kaifungue, kama ulikata tamaa kusoma kwasababu ulifeli rudi tena shule n.k

Na Mch. Godlisten Nkya