Mamlaka na Mipaka ya Kazi


MAMLAKA NA MIPAKA YA USHARIKA WA UBUNGO

Mamlaka

Mamlaka ya Usharika wa Ubungo yanatoka kwa Mungu mwenyewe, kwa katiba ya KKKT na kanuni za Dayosisi ya Mashariki  na Pwani pamoja na katiba ya nchi na sheria za nchi.

Mipaka ya kazi

Mipaka ya kazi ya Usharika inaenda sambamba na mipaka ya Dayosisi kijeografia ni Mkoa wa Dar es Salaam, sehemu ya Mkoa wa Pwani; Wilaya za Mafia, Rufiji, Mkuranga, Kisarawe, Kibaha, na sehemu ya Bagamoyo, Visiwa vya Zanzibar. Kimaudhui Dayosisi inashughulikia mambo ya kiroho na kimaendeleo.