MAHUBIRI JUMAPILI, 02-10-2016, MCHG G . NKYA
Posted in Habari on Oct 05, 2016
Bwana wetu Yesu Kristo apewe sifa
Tunaendelea kuwakaribisha watu wote wa mataifa yote,Dini zote na kabila zote katika ibada za kila jumapili hapa Kanisani Usharikani KKKT Ubungo
Pia endelea kubalikiwa na mahubili ya kila jumapili kupitia website hii,Hapa chini ni summary ya mahubili ya jumapili ya tarehe 02.10.2016
NENO:Jina la Bwana ni Ngome Imara
Yoh 1:1-5
-Vitu vyote vimekuwepo hapa duniani ,vimekuwepo kwa sababu ya uwezo wa Yesu ,pasipo yeye hapakuwepo na kitu chochote
Mathayo 16:18-19
-Mistali hii inatuonyesha nia ya Yesu ya kujenga kanisa lenye nguvu na ambalo shetani hatoliweza
Waefeso 1:22-23
-Wakristo wengi hatujafahamu nguvu iliyopa katika jina la Yesu
Marko 16
-Kwa jina langu mtatoa pepo na hata mtakapokanyaga nge na nyoka hawatawadhulu
-Ukiwa na Jina la Yesu mwanadamu ni nani ata akutishe?
TUNACHOJIFUNZA:
Tusiende ibadani kwa ajili ya kufuata utaratibu tu, bali twende ibadani kwa vile yesu yupo hapo na atatuhudumia kwa mambo yote .
Kupitia jina la Yesu tutapata muafaka wa kila jambo kwenye maisha Yetu
Tunatakiwa kujua na kukumbuka kuwa jina la Yesu ni jina lipitalo majina yote